Uongozi katika Uislamu wa Ibadhi

Kulingana na Uibadhi hata hivyo, ukoo si jambo linalohusu. Kila muumini na aliyepata mafunzo ya kitheolojia ana uwezo wa kuwa mgombeaji na anaweza kuchaguliwa kuwa imamu.

Ingawa Quran ni msingi wa falsafa zote za Uislamu, hata hivyo fasiri na maelezo, na imani zimesababisha madhehebu na mafunzo mbalimbali. Makundi yalitengana kwa mara ya kwanza baada ya kifo cha Mtume Mohammed mnamo mwaka wa 632 AD, na wafuasi wake hawakuweza kukubaliana, kama wachague warithi kutoka ukoo wake au viongozi ambao wangefuata kanuni za imani.

Tawi la Sunni walishikilia kauli kwamba Khalifa wa nne wa kwanza – warithi wa Mohammed – walichukua nafasi yake kihaki kama viongozi wa Waislamu. Wanawatambua warithi wa Makhalifa wanne kuwa viongozi wa dini. Walimchangua Abu Bakr, mshauri wa Mtume kuwa mrithi wa kwanza au Khalifa ili kuongoza taifa la Kiislamu.

Maimamu wa Suni kwa kawaida huchaguliwa kati ya wanajumuia wa kabila la Mtume Mohammed yaani kabila la Quraishi.

Kinyume cha hayo, Shia wanaamini kwamba warithi tu wa kalifa wa nne Ali (binamu yake Mohammed ambaye ni mkwe wake pia) wao ndio warithi wa Mohammed.

Ibadhi wanasisitiza kwamba kila Mwislamu mwaminifu aliyepata mafunzo ya theologia anaweza kuwa mgombea wa cheo hiki na anaweza kuchaguliwa Imanu. Imanu ni kiongozi wa dini pia wa mambo ya kilimwengu ambaye ana mamlaka yote ya serikali. Yeye ni “wa kwanza kati ya walio sawa” mbele ya macho ya Ibadhi, kama vile wanadamu ni wa kwanza kati ya viumbe wengine mbele ya mungu. Kwa hivyo umma jamii ya Waislamu huteua muumini katika tabaka lao ambaye ana sifa zinazostahili cheo hiki, kama hakuna mtu ye yote ambaye anaweza kutimiza madai ya cheo cha Imamu, basi nafasi hii hubaki tupu kwa muda fulani.

Vilevile kama Imamu aliyechaguliwa hawezi kutimiza matarajio anaweza kutolewa katika cheo hiki.

Imanu wa kwanza wa jumuiya ya Ibadhi ambaye pia ni mmojawapo wa mwanzilishi muhimu aliyehusishwa na Uibadhi ni Jabir b. Zayd (aliyefariki mwaka wa 93 AH / 711BK) Alizaliwa Nizwa katika Omani na baadaye alifanya makazi huko Iraq. Alidumisha uhusiano wa karibu na nchi asili yake ingawa kulikuwa na umbali wa kiasi fulani.

Makabila ya Al-Muhallab na Al-Azd wote walimwunga mkono kuanzisha shule (madhehebu) ya Ibadhi.

Jabir bin Zaid alimshauri Ibn Ibadhi juu ya shughuli zake nyingi za kisiasa. Wote pamoja walipinga makundi kwa mfano, Qadaria, Mutazila, Shia, Murjia na khawariji. Maibadhi wa hapo awali, walikuwa kundi la kadiri lisilozidi idadi kubwa.

Mfumo wa uimanu ulidumu mpaka mwisho wa karne ya kumi na tisa.