Kauli kihistoria

Reporti nyingi na barua za wasafiri na mabalozi wanadhibitisha kwamba Omani ilikuwa na mazoea ya falsafa ya kiamani kwa miaka mingi.

Dondoo toka kwa mwingereza John Ovington, kasisi wa mfalme James wa pili, alipotembelea Muscat mwaka wa 1633 BK:

"Hawa Warabu ni watu wenye heshima na ni wapole sana kwa wageni wote; hawafanyi vurugu zo zote zile wala hawatusi watu kwa vyo vyote; ingawa wanashikilia imara kauli zao na wanaipenda dini yao sana, hawailazimishi kwa watu wengine kwa njia yo yote ile, wala uadilifu wao siyo mioyo iliyojaa ghadhabu kwamba iwapotoshe mbali n heshima na upendo wao wa kibinadamu… Kwa ujumla hawa ni watu kadri, wenye matendo ya haki na wamejawa na ubora wa hali ya juu ambao wanafalsafa Wayunani na wadilifu Warumi walijaribu kuutia mioyoni mwa wananchi wao, lakini walikosea lengo lao."

Mfanya biashara na balozi mwamerika kwa jina Edmund Roberts, alimtembelea Sayyid Said mnamo mwaka wa 1833 na alitoa habari kuhusu mtawala wa Omani:

"Dini zote katika miliki ya Sultani hazivumiliwi tu, bali zinalindwa na mtukufu; na hakuna kikwazo cho chote kuzui Wakristo, Wayahudi au wale wasio Wayahudi, kuhubiri kanuni zao za pekee au kujenga hekalu."

Mnamo mwaka wa 1824 hahodha George Keppel, msafiri mwingereza alitembelea Muscat akiwa njiani kutoka Bara Hindi kuelekea Uingereza, yeye aliainisha Waislamu wa Omani hivi:

"Hawasujudu watakatifu na hawana jumiya za watawa wala walii. Wanaheshimu sana haki na wanavumilia dini nyingine."

Msafiri mjerumani kwa jina Carsten Niebuhr, alitembelea Muscat tarehe 3. Januari mwaka wa 1765. Akariport:

"Makundi makubwa ya Baniani kutoka Bara Hindi wamefanya makao yao katika eneo la biashara katikati ya mji. Huko Mokha wanateswa kwa kuaibishwa, lakini hapa Muscat miongoni mwa kikundi kivumilivu cha Beiasi, wanaruhusiwa kufuata Sheria na kuendeleza uabuduaji wa dini yao bila kusumbuliwa."