Mahali pa maonyesho mpaka sasa

Uonyeshaji wa kwanza wa maonyesho ulifanyika huko Ujerumani na Austria mwaka wa 2010 na siku hizo maonyesho yaliitwa “Uvumilivu wa Kidini: Uislamu katika Omani.”

Maonyesho yalipokelewa vizuri na upendeleo (shauku) ulionyeshwa katika kuonyesha maonyesho na mashirika yaliyomo nje ya eneo ambapo Kijerumani kinazungumzwa. Kwa hivyo uamuzi ulitolewa mwaka wa 2011, kutafsiri maonyesho ili yaweza kupatikana popote Ulaya.

Wakati ujumbe ulipoenea kati ya jamii ya wataalamu wa madhehebu mbalimbalil, ndipo muda wa maonyesho ulipoongezwa hadi mwaka wa 2013, ili yaweza kuonyeshwa duniani kote, na vilevile tafsiri katika lugha kumi na nane zifanywe, chini ya jina jipya “Uvumilivu, maeleowano, maingiliano: Ujumbe wa Uislamu wa Omani."