Ustahimilivu wa kidini katika Unguja

Watawala wa Omani waliokuwa na makao yao Unguja walikuwa wazi na wastahimilivu kwa Wakristo katika Afrika mashariki.

Mnamo mwake wa 1868 Sultani Majid wa Omani (1834 – 1870) aliwapatia eneo kubwa la ardhi kwa “Mapadre wa roho mtakatifu” kaskazini Bagomoyo katika bara ya pwani ili kujenga misheni ya kwanza katika Afrika mashariki. Idhini ya shamba hili ambapo misheni bado ipo, ni halisi hata leo hii.

Sultani Majid pia aliunga mkono sana kazi za mmisionari na mwanaisimu Mjerumani DK. Johann Ludwig Krapf (1810-1885) ambaye alitumwa Afrika mashariki na kanisa la “British Church Missionary Society” Alitunga sarufi na kamusi ya Lugha ya Kiswahili na kufasiri kitabu cha Agano la Kale.

Chapa za habari zilipoletwa Afrika mashariki mara ya kwanza wakati wa utawala wa Sultani Bargash (1837-1888) wamisionari waliitumia kupiga chapa fasihi za kikristo kwa lugha ya Kiswahili ili kusaidia kutekeleza juhudi zao huko bara. Walisaidiwa katika tafsiri zao na msomi mwenyeji kwa jina la Sheikh Abdel-Aziz bin Abd Al-Ghani Al-Amawi, ambaye mnamo mwaka wa 1872 alitafsiri pamoja na wengine Katekisimu na Bibilia.