Mfumo wa Sheria

Katiba ya Omani inadhihirisha Uislamu kama dini rasmi ya taifa na Sharia (ya Kiislamu) ndiyo msingi wa utungaji Sheria. Sheria zilizotungwa kuhusu mambo ya ndoa na sheria za jamii (familia) ni lazima zifuatilie misimamo thabiti ya Sharia. Sheria za kiraia na za ujinai na adhabu za mahakama ni sharti ziwe na upatanifu na sheria za kimataifa.

Usultani umeweka sahihi kwa sheria kulingana na sheria ya dola ya mataifa (UN) hasa zile zinazohusika na ulindaji wa haki za binadamu, kulindwa kwa wachache (minority) vilevile makubaliano dhidi ya aina yo yoto ile ya ubaguzi wa wanawake ha haki za mtoto.

Utawala wa sheria, mamlaka ya taifa, uhuru wa mahakama ni mojawapo za kanuni zilizowekwa ili kulinda haki za kila mwananchi wa Omani. Kila mshtakiwa anakisiwa kuwa bila hatia mpaka ithibitishwe kwamba ana hatia kupitia daawa. Utumiaji wa matusi ya kimwili au kisaikologia umekatazwa. Adhabu zo zote zile ni lazima zifuatane na sheria kwani wananchi wote ni sawa mbele ya sheria.