Asili ya jina Ibadhism

Jina Ibadhism linatokana na baba ya Abdullah bin Ibadh al-Murri al-Tamimi, ambaye alitoka katika mojawapo ya kabila kuu (maalum) la Mudar.

Yeye alikuwa mojawapo wa viongozi muhimu katika mapambano dhidi ya utawala wa Umayyad katika kulinda Maka kwa sababu aliamini kwamba utawala wa Umayyad ulivunja sheria zu Kuruni na Sunna. Katika jaribo lake la kutafuta kiongozi hodari wa kikundi hiki, alipingwa na viongozi wa wazee, kwa mfano Abdulla al-Zubair.

Kwa hivyo ilimbidi Ibn Ibadh yeye mwenyewe kuchukua nafasi muhimu katika mapambano ya kisiasa na hivyo ndivyo filosofia ya Ibadhi ilivyoibuka ikiwa na misingi halisi, mipaka iliyowekwa na ungozi. Utaratibu wa Uimamu ulidumu mpaka mwisho wa karne ya kumi na tisa.