Mazungumzo baina ya Madhehebu

Kwa muda wa miaka mingi serikali ya Omani imekuza mazungumzo kati ya madhehebu mbalimbali, ili kuendeleza uvumilivu wa kidini,uelewano wa pande mbili, na mshikamano wa amani kulingana na kiwango cha kimataifa.

Shughuli ni pamoja na mikutano ya mara kwa mara ya kimataifa, na mikutano, mihadhara, uchapishaji utoaji wa msaada kwa taasisi za madhehebu na shughuli zao.

"Hakutakuwa na amani kati ya mataifa bila amani kati ya dini, nahakutakuwa na amani kati ya dini bila mazungumzo kata ya dini mbalimbali."

Profesa Dk. Hans Küng mbele ya Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa 2001

Siku ya Kimataifa ya Uvumilivu (ustahimilivu)

Mwaka wa 1996, Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa ulialika wanachama wa Shirika la Mataifa kuchunguza Siku ya Kimataifa ya uvumilivu tarehe 16 Novemba, kwa shughuli zilizowekwa kwa wenye madaraka ya elimu na kwa wananchi wote kwa ujumla.

Ari zinazounga mkono shughuli baina ya dini mbalimbali

Serikali ya Omani inasaidia taasisi za madhehebu mbalimbali katika shuguli zao ndani ya Usultani na vilevile Ughaibuni.

Wabia wa madhebebu

Wizara ya Tunu (Fedha) na Mambo ya Kidini hushirikiana na taasisi kadhaa pote duniani katika uwanja wa kitaaluma wa mazungumzo ya madhehebu.

AL-TASAMOH, AL-TAFAHOM na ijtihadreason

AL-TASAMOH (uvumilivu) na AL-TAFAHOM (uelewano) ni majarida ya utamaduni wa kiarabu, yanayotelewa na Wizare ya Tunu na Mambo ya Kidini.