Ujumbe wa Uislamu wa Omani

Niazara ya Tunu (Fedha) na Mambo ya Dini ya Omani imekuwa ikiendeleza mazungumzo baina ya dini mbalimbali kwa miaka mingi.

"Tuna makundi matatu ya idadi ya watu katika dunia; kwanza kundi la Wakristo, Wayahudi na Waislamu wanaoamini Mungo mmoja na kitabu kitakatifu; la pili, wakanamungu ambao wamepoteza matumaini katika dini, na kundi la tatu linawakilisha dini na maoni ya kiroho mbalimbali. Tunajitahidi kudumisha mawaidha yanoyosidia mazungumzo halisi kaki ya wataalamu na wasimamizi wa makundi haya yote. Nia ya kubadilishana mawazo ni kutafakari juu ya kanuni na misingi ya mawazo yetu, uadilifu wa kawaida, busara ya kawaida juu ya haki. Ni kwa kuwa na utambuzi juu ya mifanano hii, kwani ndiyo misingi ya matendo yetu, huku tukikubali mila na utamaduni tofauti, hapo ndipo sisi na watoto wetu tutakavyoweza kufaidi maisha ya amani ya nyakati zijazo."

Sheikh Abdullah al-Salimi,
Waziri wa Wizara ya Tunu na Mambo ya Dini

Filamu

Juhudi za Omani katika uelewano na amani kati ya watu nje na ndani ya nchi inavyochukuliwa kulingana na maono ya waangalizi wa kimataifa na vyombo vya habari.

Maonyesho

Maonyesho yanayoonyeshwa duniani kukuza uvumilivu wa kidini, maelewano na maingiliano ya amani.

Mwitikio

Maonyesho hayo yanatoa utambuzi katika mazoefu ya uislamu katika maisha ya kawaida ya kila siku, uchunguzi wa maisha katika jamii ya wakati huu ya Omani na wajibu wa wanawake katika jamii.

Uibadhiya

Uibadhiya ni falsafa tofauti kuhusu Uislamu, hata Suni wala Shia, ambazo ziliibuka nyakati zu mwanzoni za Uislamu (Uibadhiya) umebaki katika mifuko ya wachache huko Afrika na ni yenye nguvu huko Omani.

Mazungumzo

Kwa muda wa miaka mingi serikali ya Omani imekuza mazungumzo kati ya madhehebu mbalimbali, ili kuendeleza uvumilivu wa kidini,uelewano wa pande mbili, na mshikamano wa amani kulingana na kiwango cha kimataifa.