Siyo upanga wala mwale - barua

Dhana zu Ulaya na Marikani kwamba Uislamu ulisambaa kwa kutumia nguvu, zinapingwa mkono na mfano wa Omani.

Mnamo mwaka wa 629 BK tarishi wa Mtume Mohammed, Amr bin Al-As, alipeleka barua kwa wana wa mfalme Julanda bin Mustakbar, yaani Abd na Jaifar. Barua zililingana na zile alizopeleka Mohammed kwa wafalme wa Byzantium, Uajemi, Uhabeshi, Misri na Yemeni. Katika barua hii aliwasihi viongozi hawa wamtambue kama Mtume wa Mungu na wasilimu.

Baada ya kushauarana na matarishi ambao walishasilimu, viongozi wa kikabila na wanasheria, wana hawa wawili wa mfalme, yaani Abd na Jaifar walikubali ombi la Mohammend na wakajiunga na kundi hili. Baada ya kusikia hayo, inasemekana kwamba Mohammed alitamka, "Mungu bariki watu wa Ghubaira. Wananiamini ingwa hawajaniona." ("Ghubaira" ni jina la zamani la Omani, ambalo bado linatumika Unguja.)