Filamu: Uvumilivu wa Kidini katika Omani

Uvumilivu ni kitu unachoweza kukiwazia, kukizungumzia, kukitolea nadharia vile unavyopenda, lakini ni kitu kinachohisiwa kibinafsi. Kupatia nafsi uzoefu huu, ni njia ya kufundishia ilivyotumiwa na mkurugenzi Wolfgang Ettlich katika mwelekeo wake wa uhifadhi wa dini na tamaduni za kiislamu za Omani. Mtazamaji huambatana na timu ya filamu kwa ziara kuhusu maisha ya kila siku katika Omani ya kisasa, kwa hivyo hupata tazamo la mara moja kuhusu sura mbalimbali za jamii, ambazo kwa kawaida huwa zimefichika kulingana na mtazamo wa wageni wa magharibi (Ulaya) Mkurugenzi ameambatana na mwomani mmoja ambaye anatoa maelezo halisi na anaeleza juu ya misingi na asili ya Uislamu. Uislamu ni dini rasmi ya Omani na ipo kote kote na inaungwa mkono na Taifa (nchi) pamoja na wafuasi wake. Madhehebu ya dini mbalimbali yanaungwa mkono pia na serikali na zinakubaliwa sana. Filamu hii inaonyesha mtazamo wa mara moja kuhusu maisha ya kidini mbali mbali yaliyomo Omani.

DVD filamu "Uvumilivuwa Dini Katika Omani" inapatikana kwa ada ndogo kupitia onilini, duka www.oman-shop.com.